KIFO CHA FIDEL CASTRO

        Kifo cha Castro aliyezaliwaAugust 13, 1926 kimetangazwa kwenye Televisheni ya Taifa na Rais wa sasa wa nchi hiyo ambaye ni mdogo wa marehemu, Raul Castro.
Akitoa tangazo la kifo cha kakake, Rais Castro, aliyeonekana kuhuzunika sana, aliliambia taifa kwenye tangazo la moja kwa moja kupitia runinga usiku kwamba Fidel Castro alikuwa amefariki na mwili wake utachomwa Jumamosi na kutakuwa na siku kadhaa za maombolezo ya kitaifa katika kisiwa hicho.
Raul Castro alihitimisha tangazo lake kwa kutamka kauli mbiu ya mapinduzi ya Cuba: “Twaelekea kwenye ushindi, daima!”

Rais wa zamani wa Cuba, Fidel Alejandro Castro Ruz.Castro alichukua madaraka ya nchi hiyo baada ya kufanya mapinduzi mnamo mwaka 1959 na kuiongoza Cuba kwa miaka 49, kabla ya kuachiangazi February 2008 na kumkabidhi uongozi mdogo wake, Raul Castro kufuatia kuugua kwa muda mrefu.

Shirika la Ujasusi Cuba (DI) limesema kwamba Shirika la Ujasusi Marekani (CIA) lilijaribu kumuua FidelCastro kwa mbinu mbalimbali mara 638, japo walishindwa kufanikisha kumuua kiongozi huyo mpaka leo ambapo Mwenyezi Mungu ameichukua roho yake
Castro amefariki dunia leo huko Havana akiwa na miaka 90.
Miaka miwili kabla, mdogo wake , Raul alishikila madaraka ya kaka yake wakati kaka yake alipofanyiwa upasuaji wa dharula wa utumbo mpana.

Baada ya Malkia Elizabeth II na Mfalme wa Thailand, kiongozi huyo wa Cuba ni wa tatu duniani kwa kukaa madarakani kwa muda murefu zaidi.Wafuasi wake wamekuwa wakiamini kuwa, Castro ndiye aliyeirudisha Cuba kwa wananchi wake huku wapinzani wakipinga uongozi wake wa kimabavu pia kwa kuwakandamiza wapinzani.

Katika miaka ya 1970 na 80, maelfu ya madaktari na walimu walikwenda Afrika na idadi sawa ya askari wa Cuba walipelekwa huko kuingilia kati migogoro na wakala wa vita baridi hasa nchini Angola.

MAMBO YA KUMKUMBUKA FIDEL CASTRO
1926: Alizaliwa Kusini Mashariki mwa Jimbo la Oriente, Cuba
1953: Alifungwa jela baada ya kuanzisha upinzani na uongozi wa Batista
1955: Aliachiliwa huru kutoka gerezani chini ya mkataba wa msamaha.
1956: Akiwa na Che Guevara, alianzisha vita dhidi ya serikali ya nchi hiyo.
1959: Aliushinda utawala wa Batista, na kuapishwa kuwa Waziri Mkuu wa Cuba
1960: Awashinda wapiganaji waliofadhiliwa na CIA waliovamia Bay of Pigs.
1962: Atifua mzozo wa makombora wa Cuba kwa kukubali USSR iweke makombora Cuba
1976: Alichaguliwa kuwa rais na Bunge la Cuba.
1992: Aliingia makubaliano na Marekani kuhusu wakimbizi wa Cuba.
2008: Aliachia madaraka ya urais wa nchi hiyo na kumkabidhi mdogo wake Raul Castro.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA ALEXANDER MASHUHURI WA UGIRIKI

HIZI HAPA MBINU BORA ZA KILIMO CHA MAHINDI

NANI MKALI KATI YA PORUS MFALME WA INDIA AU ALEXANDER WA UGIRIKI