Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2016

DAWA ASILIA ZA KUKU

Zipo dawa tofauti za asili zinazopatikana kirahisi kwenye mazingira ya vijijini ambazo zina uwezo wa kutibu magonjwa ya kuku. Katika mada hii taelezea baadhi ya dawa hizo. Dawa ya kutibu Kuku Kuharisha namna yoyote Mmea unaotumiwa ni Mpapa:Kuandaa Kata jani moja bichi la Mpapai na uliponde ponde lilainike kiasi. Kisha changanya na maji kiasi cha litambili na nusu. Kutumia (kwa tiba)- Kuku wapewe maji hayo wanywe,wasipewemaji mengine kwa ajili ya kunywa kwa siku angalau nne au zaidi.- Inafaa zaidi kila siku kuwaandalia dawa mpya ili dawa isiharibike. Kutumia (kwa kinga)- Hata kama kuku hawaharishi, wakizoeshwa kunywa maji yenye majani ya mpapai yaliyopondwa angalau mara tatu kwa wiki watakingwa magonjwa mengi.Njia nyingine ya kutumia Mpapai: Kuandaa na Kutumia- Chukua majani ya Mpapai uyatwange upate kisamvu chake kiasi cha kilo 1.- Changanya kisamvu hicho na pumba lita 2.- Waweza kuongezea maji kidogo na kuwapatia kuku wanaoumwa watumie chakula hicho hadi wapone. Kama kuku ni wach...

LOWASSA AJA NA UJUMBE MZITO

Aliyekuwa  mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kupitia Chama chaDemokrasia na Maendeleo (Chadema), Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amewashukuru wananchi kwa kumpigia kura kwa wingi licha ya baadhi kumsema vibaya kwa kumwita mgonjwa na kwamba angekufa. Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alitoa kauli hiyo mjini Mbinga mkoani Ruvuma ambako chama hicho kipo katika ziara ya kufanya mikutano ya ndani. Akizungumza ndani ya vikao hivyo, Lowassa pasipo kutaja jina la mtu yeyote alisema: “Mwacheni Mungu aitwe Mungu, kwa sababu wote hata walionisema mabaya baadhi yao wameshatangulia mbele ya haki.”Alisema kitendo cha wananchi kumpigia kura kwa wingi pamoja na kwamba alikuwa akizungumziwa vibaya juu ya afya yake, ni wazi kuwa walikubali kubeba lawama juu yake.“Bila ujasiri na umoja wa dhati, hawa jamaa wataendelea kutupiku… lakini niwashukuru vile vile kwa kukubali kubeba lawama juu yangu, wapo waliosema huyu ni mgonjwa atakufa,...

WATUMISHI WALIOSOMA CHUO KIKUU BILA SIFA KUFUKUZWA KAZI

ANAANDIKA MALISA GJ     Baada ya matamko kadhaa kadhaa ya serikali kuhusu Sekta ya Elimu nchini hatimaye leo limeibuka jingine la kutimua watumishi wote wa umma waliojiunga na vyuo vikuu na kutunukiwa "degree" bila kuwa na sifa.Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako wakati akifungua maonesho ya vyuo vya elimu ya juu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo vikuu nchini (TCU) yanayofanyika viwanja vya Karimjee, jijini Dar. Maonesho hayo yanashirikisha vyuo 61 ambapo 12 kati ya hivyo ni kutoka nje ya nchi.     Katika taarifa yake Ndalichako amesema Wizara yake inawasiliana na idara ya Utumishi ili kuwabaini watumishi wote waliojiunga vyuo vikuu bila sifa na wafukuzwe kazi.        "Kama wewe ni mfanyakazi uliyesoma moja ya vyuo vikuu ukafaulu lakini hukuwa na sifa ya kujiunga na chuo kikuu, tutakunyofoa hukohuko kwenye ajira yako" Alisema Ndalichako.       Kufuatia agizo hilo la Ndalichako, wa...

KIFO CHA FIDEL CASTRO

Picha
        Kifo cha Castro aliyezaliwaAugust 13, 1926 kimetangazwa kwenye Televisheni ya Taifa na Rais wa sasa wa nchi hiyo ambaye ni mdogo wa marehemu, Raul Castro. Akitoa tangazo la kifo cha kakake, Rais Castro, aliyeonekana kuhuzunika sana, aliliambia taifa kwenye tangazo la moja kwa moja kupitia runinga usiku kwamba Fidel Castro alikuwa amefariki na mwili wake utachomwa Jumamosi na kutakuwa na siku kadhaa za maombolezo ya kitaifa katika kisiwa hicho. Raul Castro alihitimisha tangazo lake kwa kutamka kauli mbiu ya mapinduzi ya Cuba: “Twaelekea kwenye ushindi, daima!” Rais wa zamani wa Cuba, Fidel Alejandro Castro Ruz.Castro alichukua madaraka ya nchi hiyo baada ya kufanya mapinduzi mnamo mwaka 1959 na kuiongoza Cuba kwa miaka 49, kabla ya kuachiangazi February 2008 na kumkabidhi uongozi mdogo wake, Raul Castro kufuatia kuugua kwa muda mrefu. Shirika la Ujasusi Cuba (DI) limesema kwamba Shirika la Ujasusi Marekani (CIA) lilijaribu kumuua...

UFUGAJI BORA WA KUKU WA KIENYEJI

      Napenda kumshukuru mwenyezi Mungu ambaye ameniwezesha kwa namna moja au nyingine kutoa mchango wangu kwa mtindo huu. Huu ni kama mwongozo tu wa nini utakabiliana nacho au unatakiwa kufanya katika zoezi zima la ufugaji wa kuku wa kienyeji. A.KWA NINI KUKU WA KIENYEJI? 1. Wastahimilivu wa magonjwa lakini ni muhimu wakikingwa na magonjwa ya kuku kama mdondo, ndui ya kuku n.k ili kuweza kuwaendeleza. 2. Wana uwezo wa kujitafutia chakulaardhini. 3. Wana uwezo wa kuatamia mayai, kutotoa na kulea vifaranga na ustahimilivu wa mazingira magumu kama ukame, baridi n.k 4.Nyama na mayai yake vina ladha nzuri kuliko kuku wa kisasa.(PATA SUPU YA KUKU WA KIENYEJI ILI UTHIBITISHE) 5. Wana uwezo wa kujilinda na maadui kama mwewe n.k . Pamoja nasifa hizi ni muhimu muhimu kuku haowakapewa matunzo mazuri, wakawekwa kwenye mabanda mazuri, wakapewa maji na chakula cha kutosha. B.FAIDA ZA KUKU WA KIENYEJI. Faida ni nyingi na zinafahamika lakininitaeleza zile ambazo kwa we...