Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Agosti, 2018

NANI MKALI KATI YA PORUS MFALME WA INDIA AU ALEXANDER WA UGIRIKI

Picha
Habari za jioni wakuu bila kupoteza muda niende moja kwa moja kwenye mada Natumaini wote tumeshasikia mengi sana kuhusu alexander the great ila kuna mambo machache yananitatiza na tusaidiane kujuzana kuhusu mtawala huyu.  ALEXANDER NI NANI Alexander III wa Macedonia alizaliwa 20/21 July 356 BC na kufariki 10/11 June 323 BC (Miaka 33) maarufu kama Alexander the Great aliyekuwa mfalme wa nchi ya makedonia iliyokuwa ndani ya ufalme wa kigiriki na alitumia muda wake mwingi wa maisha kupigana vita za kuteka miji mbalimbali ili kuongeza ufalme wake UMAARUFU WAKE  Umaarufu wake ulikuja baada ya kuwa mwanajeshi asiyewahi kushindwa vitani na kufikia umri wa miaka 30 alikwisha angusha falme zote kubwa zilizokuwa tishio kati ulimwengu wa kale akitandika mataifa makubwa kuanzia ulaya,Afrika hadi Asia hivyo anatazamiwa kuwa commander bora zaidi wa kijeshi katika historia. ALEXANDER AKIWA INDIA baada ya kupata picha kidogo ya nani anazungumziwa twende moja kwa moja kwenye swali l...

HISTORIA YA ALEXANDER MASHUHURI WA UGIRIKI

Picha
Alexander III wa Macedon (20/21 July 356BC-10/11 June 323BC), alijulikana kama Alexander the Great, alikuwa Mfalme wa Ugiriki falme ya Macedon na pia mmoja wa wanafamilia wa family ya Kifalme ya Ugiriki (Agead dynasty). Alizaliwa mjini Pella mwaka 356 BC, Alexander alimrith baba yake Philip II, katika ufalme akiwa na umri wa miaka 20. Alitumia muda wake mwingi wa utawala katika kuongoza majeshi yake kwa upana na urefu kupitia Asia na North Africa, akiwa na miaka 30 alikuwa amejijengea moja katika falme kubwa katika historia ya dunia, iliyotokea Ugiriki mpaka India. Hakuwahi kushindwa katika vita na inaaminika mpaka leo kuwa ni komandoo wa jeshi ambae hajawahi kutokea. Katika ujana wake, Alexander alikuwa mwanafunzi wa mwanafilosofa Aristotle mpaka kufikia umri wa miaka 16. Aristotle ni mwanafilosopher ambae kanuni zake za ethics bado zinatumika katika ulimwengu wa leo, katika masomo Alexander aliyosoma ilkiuwa ni pamoja na biology, zoology, physics, logic na mengineyo. Baada ya kuuwaw...