Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2018

KILIMO CHA ALIZETI

Alizeti hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara, na Rukwa. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara. MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA UZALISHAJI Kuchagua aina bora ya mbegu - Chagua aina bora ya mbegu inayovumilia magonjwa, wadudu, inayotoa mazao mengi na kiwango kikubwa cha mafuta. - Vilevile chagua aina ya mbegu ambayo hukomaa kwa wakati mmoja ili kurahisisha uvunaji. KUWEKA MBOLEA - Rutubisha udongo kwa kutumia mbolea za mboji na samadi ili kupata mazao mengi na bora. KUDHIBITI WADUDU NA MAGONJWA Alizeti hushambuliwa na magonjwa ya majani, mizizi na masuke ambayo husababisha upungufu wa mavuno. Hivyo ni muhimu kuyadhibiti ili kupata mavuno mengi na bora. Pia ndege hupunguza mavuno kwa kiasi cha asilimia 50 au zaidi. Njia ya kudhibiti ndege ni kwa kuwafukuza na kupanda mbegu zinazokomaa mapema. MAANDALIZI KABLA YA KUVUNA; UKAGUZI Kagua shamba kuona kama alizeti imekomaa. Alizeti hu...

KILIMO CHA KAROTI

Karoti ni zao la mbogamboga ambalo ni zao mizizi, kwa kawaida hupatikana katika rangi ya machungwa,  nyekundu, njano. Karoti za sasa zimetokeza kutokana na karoti pori, Daucus carota. Karoti hutumika sana kwaajili ya kuongeza radha kama kiungo kwenye mboga au kwenye kachumbari na pia zinafaida kubwa katika mwili kwa kukupatia vitamin A na C pamoja na madini ya chuma hasa pale mtu atafunapo. HALI YA HEWA NA UDONGO. Karoti zinahitaji hali isiyokuwa na joto sana, wala baridi sana, kati ya nyuzi za degree 15 mpaka 27 za sentigredi. Kama ukanda wa pwani una joto kali, inatakiwa karoti zilimwa miezi ya majira ya baridi, karoti zinazotoka mazingira ya baridi huwa na radha nzuri pamoja na harufu nzuri. Udongo wa kichanga chepesi na tifutifu ndio unafaa katika kilimo cha karoti, udongo wa mfinyanzi na udongo mzito hudumaza mazao. UTAYARISHA WA SHAMBA Karoti zinahitaji Shamba la Karoti lilimwe kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45 kwenda c...

KISA CHA ABUNUWASI NA MFALME

SIKU moja alfajiri, wakati wananchi wa mji wenye wakazi wengi walipokwenda kuchota maji mtoni, walishangazwa kuuona mkono wa mtu ukiwa katikati ya mto. Mkono huo wa ajabu ulikuwa umenyoosha vidole viwili juu, kuonyesha alama ya mbili. Wananchi walistushwa sana na kitendo hicho, wakaogopa hata kuchota maji mtoni, kwani hawakuwahi kuona tukio la kuogopesha kama lile. Wengine waliamini kuwa huo ulikuwa mwili wa mtu aliyetupwa mtoni. Lakini ishara iliyoonyeshwa na mkono huo iliwafanya wananchi waamini kuwa huo ulikuwa mkono wa ajabu. Katika kiza kinene kilichozunguka ndani ya vichwa vya wananchi, habari zikamfikia Mfalme wao, naye akafika haraka eneo la tukio. Mfalme wa nchi hiyo baada ya kujiridhisha kuwa ulikuwa mkono wa ajabu na uliwekwa na watu wenye imani za kishirikiana, alitoa siku tatu mkono huo uwe umeondolewe, vinginevyo ataleta wataalam kutoka sehemu mbali mbali duniani kwa ajili ya kubaini wahusika. Siku tatu zilizowekwa na Mfalme zikaisha, wataalam wa mambo ya asili kutok...

SIMULIZI :HILI NI JIJI LA NEWYORK

Picha
Kila Mmarekani alikuwa na shauku ya kuitazama timu yao ya mpira wa kikapu ya New York Buckets ambayo ilikuwa ikitarajiwa kushiriki mashindano ya dunia ya klabu ya mpira wa kikapu ambayo yalitarajiwa kufanyika, Shanghai nchini China wiki inayofuata. Kwa wakati huo hakukuwa na ushabiki wa timu moja tena, mashabiki wale ambao walikuwa wakiishabikia La Lakers, Chicago Bulls na timu nyingine katika Ligi ya NBA wakaunganisha nguvu zao kwa kuipa nguvu timu ya New York Buckets ili iweze kushinda mashindano hayo ya dunia. Idadi kubwa ya Wamerekani hasa wale waliokuwa wakipenda mchezo wa kikapu wakawa na bendera nyingi za New York Buckets mikononi mwao. Waandishi wa habari hawakuwa mbali, kila wakati walikuwa wakirusha kwenye televisheni mbalimbali mazoezi ambayo yalikuwa yakifanyika katika uwanja wa mazoezi ambao ulikuwa katikati ya Jiji la New York, The Margedonians. Ingawa Waingereza mara kwa mara walikuwa wakiitangaza timu yao ya mpira wa kikapu ya The Buffalloes lakini wakaonekana kuanza...